safina women

WOMEN HAVE THE RIGHT TO OWN LAND

TAARIFA YA UZINDUZI WA MATOKEO YA UTAFITI WA ELIMU (TWAWEZA)

Shirika la SAFINA Women Association la Njombe lilishiriki kufanya tathmini inayoendeshwa na TWAWEZA EAST AFRICA kupitia UWEZO mwaka 2015, katika Halmashauri ya Mji Njombe. Tathmini hiyo ilifanyika tarehe 16 na 17/10/2015 katika maeneo 30 ya utafiti, zilifikiwa shule 30 na kaya 600. Baada ya tathmini kukamilika taarifa ilipelekwa UWEZO kukamilisha kuunganisha taarifa hiyo Kitaifa.

Tarehe 24/10/2017 tulipokea taarifa ya majumuisho ambayo iliandaliwa tayari kwa uzinduzi kwenye tukio muhimu likiwakilishwa na wadau mbalimbali wa Elimu.

UZINDUZI WA RIPOTI YA UWEZO:-

Tarehe 9/11/2017 ulifanyika uzinduzi wa taarifa ya tathmini katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Njombe. Washiriki walifika kuanzia saa 6:30 Mchana. Mgeni rasmi aliingia Ukumbini mnamo saa 7:15.Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ndugu Ruth B. Msafiri. Waalikwa wengine walioshiriki ni mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Mji, mwakilishi wa Mbunge, Katibu Tarafa, Afisa Elimu shule za Msingi Njombe Mji, Madiwani wawili (2), Waratibu Elimu Kata wawili (2), Katibu Kata wawili (2), Katibu wa Chama cha Waalimu, Viongozi wa NGOs wadau wa Elimu, Waalimu, Wazazi Wahojajisita(6)Wasimamizi wa Wahojaji watatu(3) naWanafunzishule za Msingi Kumi na mmoja (11).
download full report

Submit a Comment

Your email address will not be published.